Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limejipanga kumaliza kero ya makazi ya nyumba kwa watanzania ifikapo mwaka 2025.

Hayo yamesemwa na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), Erasto Chilambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Ili kutimiza azma hiyo, Chilambo amebainisha kuwa nyumba zisizopungua elfu 30 zitajengwa kwa ajili ya kuuzwa na kupangishwa ambapo katika nyumba hizo watu wa kipato cha chini, kati na juu ndio walengwa.

“Katika mkakati huu, Shirika limekusudia kujenga nyumba 12000 kwa ajili ya watu wa kipato cha chini, nyumba 13500 kwa ajili ya watu wenye kipato cha kati na nyumba 2700 kwa ajili ya watu wenye kipato cha juu.” Amesema Chilambo.

Aidha, Shirika linajenga majengo 1800 ya kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini, ambayo yanatazamiwa kukamilika ifikapo 2025.

Hata hivyo, Tangu kuanzishwa kwake Shirika la Nyumba limekuwa likimiliki na kuuza majengo mbalimbali, na hivi sasa shirika linamiliki Majengo 2483 yenye sehemu 18121 za makazi na biashara katika Mikoa ya Tanzania Bara.

Klopp, Wenger Hawana Uwezo Wa Kufundisha FC Barcelona
Serikali yatoa msimamo kulinda kazi za filamu nchini