Kampuni ya Magari ya AMC Tanzania ambao ndio wauzaji pekee wa magari aina ya Nissan imetoa msaada wa Mabegi na Kompasi Shule ya Viziwi Buguruni.
Akikabidhi vifaa hivyo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Christopher Henning amesema kuwa wamejisikia fahari kusaidia wanafunzi 237 wenye mahitaji maalum.
Amesema kuwa kampuni yake itakaa katika meza tena na uongozi wa shule hiyo kuona namna ya kuisaidia kwa kipindi hiki ambacho inatimiza miaka mitano tangu kufunguliwa nchini.
“Kama sehemu ya wajibu wetu wa kurejesha faida hii kwa jamii, tumeona tujikite kusaidia wenye mahitaji maalum hasa watoto ili waweze kupata elimu katika mazingira bora kwani tunaamini viwili (watoto na elimu) hivyo ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi yetu.” amesema Henning.
Amevitaja vifaa hivyo, ambavyo kampuni hiyo imevitoa kwenye shule hiyo kuwa ni pamoja mabegi na Kompasi za kutumia wanafunzi hao.
Aidha, katika hotuba yake mtendaji huyo ameahidi kuwa Nissan Tanzania itaendeleza ushirikiano na shule ya Buguruni kwa manufaa ya pande zote mbili ili kuleta ustawi katika jamii.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Kulwa Milembe amesema kuwa wanafunzi wake wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo vifaa vya kubebea vitu wanafunzi ambao wengine wametoka nje ya jiji la Dar es salaam na familia zao ni duni sana.
-
Video: Ukurugenzi Morogoro kaa la moto, JPM ahofia wa kuendeleza miradi
-
Serikali kujenga bweni la kisasa la wanafunzi wenye mahitaji maalum
Pamoja na msaada huo, ameiomba kampuni hiyo kuendelea kusaidia wanafunzi wake ili waweze kusonga mbele katika elimu. ambapo shule hiyo yenye wavulana 110 na wasichana 127 na kufanya jumla yao kuwa 237 ina vitengo vya msingi, ufundi, awali na wasioona.