Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare amesema baada ya kukatika kwa mawasiliano ya Barabara kuu ya Dodoma- Morogoro eneo la Kiegeya, wilaya ya Kilosa, watumiaji wa Barabara hiyo kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda Dodoma watumie njia ya Iringa.

“Kwa hali ya sasa magari hayawezi kupita hivyo wanaotumia Barabara hii ninawataarifu wananchi wabaki kwenye maeneo yao kwa kuwa Serikali ipo katika kurejesha maeneo hayo kama hapo awali “amesema Sanare

Kazi ya matengenezo ya daraja hilo imeanza tangu usiku kwa kuweka vifusi na mawe huku madaraja mawili ya chuma yakiwa yanatengenezwa na jeshi la wananchi (JWTZ).

Naibu waziri wa ujenzi, Elias Kuandikwa ametembelea eneo hilo leo Machi 3, 2020 na kubainisha kuwa juhudi mbalimbali zimeanza na ujenzi wa madaraja mawili ya chuma.

Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inafanya matengenezo kwa haraka ili mawasiliano yaweze kuendelea kwani barabara hiyo inategemewa kiuchumi si kwa mikoa ya kanda ya kati na ziwa pekee bali hata maziwa zikiwemo Uganda, Burundi na Congo.

Dkt. Shein afurahishwa taarifa ya BOT Zanzibar
Vijana wa " Ile pesa tuma kwenye namba hii" wakamatwa Mbeya