Mtoto mwingine anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 7-10 aliyefahamika kwa jina la Rechael Malekela mkazi wa kijiji cha Matebwe wilayani Njombe mkoani humo amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali mita chache kutoka nyumbani kwao.

Akithibitisha tukio hilo, mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema kuwa ni kweli mtoto huyo amekutwa amefariki na walipata taarifa hizo.

“Mtoto huyo amechomwa chomwa na vitu vyenye ncha kali nadhani mtoto huyu alikuwa peke yake akitoka kwa mama yake na kuelekea kwa kaka yake, hapa katikati kuna kama umbali wa hatua 500 ambazo zinatenganisha na hapa kuna kama kamsitu fulani na ndio alivamiwa na kupata madhara na huyo mama alikuwa shambani, shamba ambalo lipo mbele ya nyumba na nyuma ya nyumba kuna hako kamsitu,”amesema DC Msafiri

Katika hatua nyingine Watu wawili wilayani Ludewa mkoani Njombe wameuawa kwa kuvamiwa na wananchi wenye hasira kali kwa madai kuwa ni miongoni mwa watu wanaohusika na mauaji ya watoto wadogo mkoani humo.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Ludewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo, Andrew Tsele amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, huku akisema kuwa miongoni mwa marehemu ambaye ni mkazi wa kijiji hicho anafahamika kwa matukio ya wizi.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 3, 2019
Uganda: Wafungwa waliofanya mitihani gerezani wafaulu