Zaidi ya asilimia 95 ya wafungwa waliofanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne (UCE) mwaka jana nchini Uganda, wamefaulu kuendelea na masomo ya Advanced level na wengine kujiunga na vyuo vya ufundi.

Kwamujibu wa baraza la mitihani la taifa Uganda (UNEB), matokeo waliyoyatoa jana jumla ya wafungwa 38 kati ya 43 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa madaraja ya pili hadi ya nne.

Kati ya wafungwa waliofaulu wanne ni wanawake, wafungwa saba wamepata daraja la pili, 20 daraja la tatu, 11 daraja la nne na mmoja amepata daraja la saba wengine watatu hawakufanya mtihani.

Tom Kitutu, mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la mauaji ndiye aliye ibuka kinara kwa wafungwa wote katika mitihani hiyo, na ameahidi kuendelea na elimu ya advanced level ili kutimiza ndoto yake yakuwa mwanasheria.

” Nilipo ingia gerezani nilitambua umuhimu wa elimu, niliungunishwa na marafiki na sasa naona kuwa elimu ndiyo njia pekee ya kuongeza thamani katika maisha yangu hapa gerezani na baada ya kumaliza kifungo changu” aliongoza Kitutu.

Mkuu wa Shule waliyosoma wafungwa hao Gilbert Nawamanya ameeleza kuwa ufaulu wa mwaka 2018 ni mzuri na amewasifu watahiwa wake kuwa na nidhamu ya haliyajuu kipindi chote cha masomo licha yakuwa ni wafungwa na anauhakika watafanya vizuri hata katika elimu ya juu.

Nakuongeza kuwa moja ya changamoto waliyokuwa wanakutana nayo nipale wafungwa wanapotakiwa kuwa mahakamani muda wa masomo.

Aidha amesema wanaunzi hao wamefanya vizuri katika masomo ya History, Geography na Commerce huku wakifanya vibaya katika Physics na Mathematics.

Kwa upandewake msemaji wa Gereza ameelezea ufaulu huo kuwa ni kupiga hatua kwani kuwapa elimu wafungwa kunasaidia kupunguza kiwango cha wahalifu nchi humo, ambapo wakitoka wanakuwa na kazi maalum za kufanya.
 

 

 

Njombe bado hali tete mauaji ya watoto
VIDEO: Inaaminika Bundi ‘ALIYETUA BUNGENI’ ni tiba kiboko, dawa ya vita, mkosi…