Nyasi bandia zitakazowekwa kwenye uwanja wa mkongwe wa Nyamagana uliopo mjini Mwanza zimewasili katika ofisi za Shirikisho la Soka nchini TFF.

Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amesema nyasi hizo zilizokuwa zimezuiwa kwa takriban mwaka mzima katika bandari ya Dar es salaam, kwa sababu ya ushuru, tayari wamezipokea.

“Hivi ninavyozungumza na wewe, tayari kontena mbili za nyasi bandia na vifaa vyake vyote zipo hapa makao makuu ya TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na wakati wowote zitasafirishwa kwenda Mwanza,”amesema.

Alfred amesema kwa sasa wanasubiriwa wataalamu tu kutoka China au Ujerumani ili waende kuzitandika nyasi hizo bandia kwenye uwanja wa Nyamagana.

Uwanja wa Nyamagana

Katika hatua nyingine, Alfred amesema shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limatoa taarifa ya ujio wa maafisa wake kuja nchini kwa ajili ya kukagua Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, ili kuupitisha tena kwa matumizi ya michezo ya kimataifa.

Simba SC, Yanga SC Waukubali Uwanja Wa Uhuru
Jose Mourinho Awakebehi Mashabiki Wa Liverpool