Mlinda mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern, Munich Oliver Kahn ameteuliwa kuchukua nafasi ya mwenyekiti mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Karl-Heinz Rummenigge kuanzia Januari 2022.
Kahn ambaye hivi sasa ni mfanyabiashara na mtaalamu wa masuala ya michezo katika runinga, amekuwa akitajwa kwa mara kadhaa kuchukua nafasi ya Rummenigge mwenye umri wa miaka 63, ambaye atajiuzulu wakati mkataba wake utakapofika kikomo Disemba 31, 2021.
“Ni heshima kubwa kwangu kwamba nitaaminiwa kushika wadhifa katika ofisi kama mwanachama wa bodi ya bayern Munich na baadaye katika ofisi ya mtendaji mkuu CEO na mwenyekiti wa bodi ya utendaji ya Bayern Munich,” alisema Oliver Kahn.