Msanii wa muziki wa bongo fleva Ali Saleh Kiba amesema katika maisha yake hawezi kuishi maisha ya kistaa kama walivyo wanamuziki wengine hapa nchini na nje ya nchi.

Amesema hayo alipoulizwa na waandishi wa habari anawezaji kutofautisha maisha ya familia na ya kazi ya sanaa, wakati wa uzinduzi wa filamu ya msanii wa bongo movie Ahmed Salim maarufu Gabo.

Mkali huyo wa kibao cha ‘seduce me’ alisema kuwa maisha ya kuigiza hayajui ila akiamua kuyafanya watu watamuogopa na kila saa kamera za waandishi wa habari zitakuwa kwake, isipokuwa hapendi tabia hiyo.

Amesema kuwa anafurahi maisha ambayo anaishi sasa ivi anapata muda wa kukutana na mashabiki wake kwa ukaribu ndio maaana ameweza kutofautisha maisha ya muziki na familia.

Wolper acharuka warembo bongo movie kutumika kingono na waandaaji
Oliver Kahn arejea Bayern Munichen