Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniface Butondo ameibana Serikali ieleze ni lini kituo cha afya cha Nhobola kitafanyiwa ukarabati baada ya kuwa chakavu kwa kipindi kirefu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa kituo hiko wakati alipokuwa akiongea hii leo Aprili 25, 2024 Bungeni jijini Dodoma.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amesema kituo cha afya cha Nhobola ni miongoni mwa vituo vya afya 202 kongwe, ambavyo vinahitaji ukarabati mkubwa, ili kuendana na mahitaji ya sasa ya utoaji wa huduma za afya.

Amesema, Serikali itavifanyia ukarabati vituo hivyo kwa awamu kikiwemo kituo cha afya Nhobola katika Halmashauri ya Kishapu.

Wakala wa Ben White awakosoa wakosoaji
Fred Funga Funga amuibua Ahmed Ally