Wakala wa Mshambuliaji kutoka Argentina Paulo Dybala anatarajiwa kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Klabu ya AS Roma Tiago Pinto, kuhusu mustakabalimchezaji huyo, ambao unaweza kuhusishwa na ule wa Jose Mourinho.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliwasili kama mchezaji huru msimu uliopita wa joto baada ya kuondoka Juventus na mkataba wake unaendelea hadi ifikapo Juni, mwaka 2025, lakini kuna kipengele cha kutolewa kinachoaminika kuwa cha Euro milioni 20 kwa timu za Italia na Euro milioni 12 klabu nje ya Italia.

Licha ya matatizo mengi ya majeruhi, bado aliweza kuchangia mabao 17 na pasi nane za mabao katika mechi 37 za mashindano na kuwasaidia kutinga Fainali ya Ligi ya Europa, ambayo walipoteza kwa Sevilla kwa Penati.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vikiwamo Calciomercato.com na Sky Sport Italia, wakala, Jorge Antun tayari yuko Roma kwa ajili ya mazungumzo na Uongozi wa AS Roma.

Mkutano huo utakuwa chini ya Mkurugenzi wa Michezo, Tiago Pinto, mapema juma lijalo na mustakabali wa Dybala unaweza kuhusishwa na ule wa Mourinho, ambaye anasubiri mazungumzo.

Sanamu ya Mwl. Julius k. Nyerere kujengwa Ethiopia
David de Gea mguu ndani, mguu nje Man Utd