Maneje wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, Pep Guardiola, ametaka Kiungo kutoka nchini Ubelgiji Kevin De Bruyne arejee kwenye misingi yake ili kuwa katika kiwango chake bora.

Mchezaji huyo bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu England, alikosa michezo miwili kutokana na kuwa majeruhi.

Mbelgiji huyo hakuwa na kiwango kizuri dhidi ya Newcastle United katika ushindi wa mabao 2-0 siku ya Jumamosi (Machi 05) na alibadilishwa na Bernardo Silva.

De Bruyne alipata matokeo mazuri baada ya kufunga bao zuri katika ushindi wa mabao 3-0 wa City wa Kombe la FA dhidi ya Bristol City juma lililopita, lakini Guardiola amesema hakuwa kwenye ubora wake.

“Kila mtu anakijua kiwango chake, ndani ya juma moja ana nafasi ya kuonyesha ubora wake, amefurahishwa na ushindi tulioupata, hiki ndicho tunachotakiwa kufanya. Turudi kwenye kanuni, tufanye kazi kwa bidii.”

De Bruyne amefunga mabao manne na kutoa asisti 12 kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu, huku City wakishika nafasi ya pili, alama tano nyuma vinara Arsenal.

City wana mapumziko ya katikati ya juma bila kucheza mchezo wowote na kuwaruhusu wachezaji kupumzika ili kupata nafuu kabla ya safari ya Jumamosi ya ligi dhidi ya Crystal Palace na kisha kuwakaribisha RB Leipzig katika mchezo wa Mkondo wapili Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Tunajiandaa vema kwa ajili ya mchezo dhidi ya Crystal Palace, kila mara ilikuwa ngumu kwetu,” amesema Guardiola.

Serikali kumlipa mshahara Adel Amrouche
Carlo Ancelotti: Bado tunatetea ubingwa La Liga