Mwimbaji Rita Ora amelazimika kupumzika kwenye vitanda vya hospitali moja Los Angeles Marekani baada ya afya yake kushindwa kuhimili kazi kubwa anayoifanya kusaka pesa.

Mwimbaji huyo amepost tweet yenye picha inayoonesha akiwa ametundukiwa drip za maji na dawa hospitalini.

Kupitia tweet hiyo, aliwashukuru mashabiki wake kwa mapenzi waliyomuonesha na kueleza kuwa hali hiyo ilitokana na kuwa na siku nzito.

”Leo ilikuwa siku ngumu lakini naendelea nayo vizuri, asanteni wote kwa kuniunga mkono! Nawapenda!! ##exhaustionisreal (sic) inasomeka tweet ya Rita Ora aliyoiandika kiingereza.

Hali hiyo imemkuta mwimbaji huyo anayeonekana kuwa na ratiba nzito ya kufanya kazi, ikiwa ni wiki moja tu baada ya kusaini dili kubwa na Atlantic Records ya Uingereza.

Video: 'Wasanii wengi wanaamini kupitia mimi' - Darasa
Video: Uharibifu uwanja wa Taifa, Yanga kuwajibishwa