Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamekamilisha maandalizi ya kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Simba SC imekamilisha maandalizi hayo chini ya ukufunzi wa kocha mkuu Didier Gomez akisaiana na kocha mzawa Seleman Matolla.

Simba SC na Al Ahly wanakutana katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa Kundi A kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kesho Jumanne (Februari 23), huku kila mmoja akiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo uliopita.

Simba SC ilishinda mchezo wake wa kwanza kwa bao 1-0 ugenini dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo wakati Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi, iliifunga Al Merrikh ya Sudan mabao 3-0 mjini Cairo.

May be an image of 1 person, playing American football, standing and grass
May be an image of 2 people, people standing, people playing American football and grassMay be an image of 2 people, people standing, people playing American football and grassMay be an image of 1 person, standing, playing American football and grass
May be an image of 1 person, standing, playing American football and grass
May be an image of 1 person and playing a sport
PICHA: KMC FC yaivutia kasi ASFC
Wakamatwa kwa kueneza uvumi juu ya Corona

Comments

comments