Ni dhahiri kuwa Rais John Magufuli ni mtu wa watu asiye na majivuno na asiyetabirika hata kidogo.

Leo, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe mama Janeth aliungana na viongozi wengine wa Jiji la Mwanza na kula kwenye mgahawa mmoja ulioko nje ya uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupata nafasi ya kuzungumza nao wakati huo.

Magufuli Mgahawani 2

Dk. Magufuli alitua katika uwanja huo wa Mwanza akielekea nyumbani kwao, Chato mkoani Geita. Alipumzika kwa muda katika uwanja huo na kupata chakula cha mchana kwenye mgahawa ambao haukutarajia kupata ugeni mzito mchana huo.

Waliompiga Daktari Washushiwa Rungu
Tanzania yanyimwa Trilioni Moja kwa uchaguzi wa Marudio Zanzibar