Ndugu wa mgonjwa wanaodaiwa kumpiga daktari wa Hospitali ya Mkoa ya Ligula mjini Mtwara wamekumbwa na mkono wa sheria kufuatia kitendo hicho.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe amesema kuwa jeshi hilo linawashikilia watu wawili wanaoaminika kuwa ndio waliotekeleza tukio hilo.

Alisema kuwa watu hao wa walikamatwa juzi usiku na kwamba Jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wengine watatu wanaohusishwa na tuhuma hizo.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia watoto na Wazee Ummy Mwalimu alifika aktika Hospitali hiyo kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro uliotokana na tukio hilo, baada ya madaktari wa Hospitali hiyo kugoma kufanya kazi wakilaani kitendo hicho.

Madaktari hao waliitaka serikali kuhakikisha kuwa mazingira yao ya kazi yanakuwa na usalama na amani ndipo waweze kuendelea na utoaji huduma.

 

Uliiona hii Video? Raila Odinga aanguka na Jukwaa akisimulia ya 'Yesu na Shetani'
Picha: Magufuli ashtukiza tena, apata chakula kwenye Mgahawa