Kikosi cha Young Africans kinachonolewa na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic kimeondoka jijini Dar es salaam leo asubuhi, kueleleka mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Jumapili, Septemba 27.

Meneja wa Young Africans, Hafidh Saleh amesema kikosi kimeondoka na wachezaji 25 ikiwa ni pamoja na wale wanne ambao walikosa mchezo wa mzunguuko watatu dhidi ya Kagera Sugar waliokubali kufungwa nyumbani bao moja kwa sifuri mwishoni mwa juma lililopita.

Wachezaji walioukosa mchezo huo ni Abdalah Shaibu,’Ninja’, Paul Godfrey,’Boxer’ Juma Mahadhi na Farouk Shikalo.

KMC FC kucheza na Kagera Sugar Kaitaba

“Tunakwenda na wachezaji wetu wote tuliowasajili 25 kwa gari na tutapata muda wa kufanya mazoezi ili kujiweka sawa, lengo ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,” amesema.

Mtibwa Sugar inawakaribisha Young Africans msimu huu 2020/21 ikiwa imetoka kushinda bao moja kwa sifuri dhidi ya Ihefu FC Uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya.

Panya buku wa Tanzania apata nishani ya dhahabu Uingereza
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 25, 2020

Comments

comments