Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Karim Benzema amefunguliwa mashtaka, kufuatia tukio la kuvujisha picha chafu za video, zinazomuhusu mshambuliaji wa klabu ya Olympic Lyon Mathieu Valbuena.

Msimamizi wa kesi inayomuhusu mshambuliaji huyo, amesema Benzema alitiwa nguvuni na jeshi la polisi na tayari ameshatoa maelezo ya awali kufuatia tuhuma zilizoelekezwa dhidi yake ambazo zinachukuliwa kama udhaifu ambao huenda ukatumika kushusha morari ya uchezaji wake wa soka anapokua uwanjani.

Benzema, mwenye umri wa miaka 27, anadaiwa kuvujisha picha za video za Valbuena, bila kumuhusisha muhusika hali ambayo ilipelekea jeshi la polisi kuingilia kati kutokana na mashitaka yaliyofikishwa mezani kwao.

Hata hivyo imeelezwa kwamba wawili hao ni marafiki wa karibu, na hatua hiyo ilichagiza picha hizo kumfikia kwa urahisi Benzema.

Benzema alikamatwa siku ya jumatano nchini Ufaransa.

Garde: Nimeshawishiwa Na Gerard Houllier
Wapinzani Zanzibar Wagawanyika