Shirika la kutetea haki za binaadamu Amnesty International, limesema, takriban watu 28 walinyanyaswa kingono na Polisi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali ya Colombia mwaka jana.
Kesi 28, ambazo zilitokea kati ya Aprili 28 na Juni 30, 2021 zilisajiliwa katika miji saba ikiwemo mji mkuu wa Bogota, baada ya Amnesty International kupokea mamia ya ripoti za unyanyasaji wa kijinsia wakati wa vurugu hizo.
Aidha, taarifa hii inakuja wakati maelfu ya watu waliokabiliwa na mzozo wa kiuchumi uliosababishwa na janga la Uviko-19 wakiingia barabarani kupinga nyongeza ya ushuru iliyopendekezwa na Rais wa wakati huo, Ivan Duque ambayo ilisababisha ajiuzuru.
Hata hivyo, ripoti hiyo inaelezea matukio mengi ya Polisi, ikiwa ni pamoja na kusambaza gesi ya machozi na hatua nyingine za kutawanya umati kwenye mikusanyiko ya amani, kuwatenga wanawake na kuwashambulia.