Jeshi la Polisi limetoa tamko kuhusu tangazo la Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuwa kesho wamepanga kufanya maandamano hadi Ikulu kwa lengo la kuishinikiza serikali kubadili msimamo wake kuhusu TBC kutorusha Live baadhi ya vikao vya Bunge.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro amepiga marufuku maandamano hayo na kuwataka vijana hao kutumia njia mbadala za kupata ufumbuzi wa suala hilo badala ya maandamano.

Akitoa sababu za kuzuia kufanyika kwa maandamano hayo, Kamanda Sirro alisema kuwa hakuna taarifa kuwa kesho na pia hakuna uthibitisho kuwa maandamano hayo yatapokewa na Rais Magufuli.

Pia, Kamanda Sirro alieleza kuwa BAVICHA hawakuanisha barabara ambazo wanatarajia kutumia katika maandamano hayo.

“Siku hiyo sio nzuri sana kwa sababu ni siku ambayo watu wanakuwa kazini. Ni siku ambayo wengi watataka kutumia barabara hizo kwa ajili ya huduma za kijamii. Na kwa sababu kuna option nyingine ya kuweza kupata suluhu hiyo, nisema tu kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku,” alisema.

Baada ya Mbunge wa CCM kutaka Bangi ihalalishwe, Daktari aeleza faida na hasara zake kiafya
Azam FC Kuzileta Dar es salaam Zesco, Zanaco