Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amehudhuria mkutano wa wataalamu mbalimbali Barani Afrika utakaofanyika Kigali nchini Rwanda ambapo watajadili masuala ya maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) husasani katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika mkutano huo, Prof. Mbarawa amemwakilisha Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Magufuli ambapo mkutano huo unatakuwa ni wa siku mbili.

Aidha, Prof. Mbarawa ataelezea kwa kina changamoto na mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania katika uwekezaji wa Miundombinu ya Habari na Mawasiliano, Maendeleo ya Sera na Miongozo inayotumika hapa nchini katika kusimamia sekta hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuiunganisha Tanzania na Mataifa mengine.

 

TFF Yavitahadhalisha Vyombo Vya Habari Kuacha Kampeni Chafu
Wenger Awachokonoa Wajumbe Wa Bodi