Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania – TCU, kusimamia vyuo vyake kufanya tafiti katika maeneo bobezi yanayotatua changamoto za kijamii na kuyachapisha kwenye majarida ya kimataifa.

Profesa Mkenda ameyasema hayo wakati akifungua maonyesho ya 18 ya vyuo vikuu nchini yenye kaulimbiu “Kukuza ujuzi nchini kupitia elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia kwa uchumi imara na shindani” huku pia akiiagiza TCU kudhibiti ubora wa vyuo, ili mitaala itakayokuwepo ijibu mahitaji ya soko.

Amesema, “TCU isimamie tafiti na kutoa ushauri kwa vyuo ili vitoe majibu ya changamoto yanayoikabili jamii, wanapaswa kuimarisha ushirikiano na taasisi za utafiti na sekta binafsi, kuweka utaratibu wa kuendeleza teknolojia na kuhamasisha matumizi, ili kupata maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya TCU, Profesa Penina Mlamba alisema wataendelea kusimamia vyuo kutoa elimu yenye tija kwa wahitimu na Taifa kwa ujumla, na kwamba pia wataendelea kuboresha maonesho hayo, ili kuzifanya taasisi za elimu ya juu kuwa chachu kwa maendeleo.

Hospitali ya Bombo kuwa kituo cha urekebishaji viungo
Paris Saint-Germain wavamia dili la Harry Kane