Klabu ya Arsenal huenda ikaachana na mpango wa usajili wa mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England, Leicester City, Jamie Richard Vardy kufuatia harakati walizozianza hii leo za kumfuatilia mpachika mabao wa klabu ya Spartak Moscow ya Urusi, Quincy Promes.

Arsenal wameanza kumfuatilia mshambuliaji huyo kutoka nchini Uholanzi, baada ya siku kadhaa kupita ambapo taarifa za Vardy kubaki King Pawer Stadium kuchukua nafasi kubwa katika baadhi ya vyombo vya habari.

Vardy, bado anasubiriwa kutoa jibu la mustakabali wake kama atajiunga na Arsenal ama kubaki na klabu ya Leicester City, baada ya Arsenal kuwasilisha ofa ya Pauni milioni 20 majuma mawili yaliyopita.

Hata hivyo The Gunners wameingia katika mawindo ya kumsajili Promes huku wakikuta upinzani mkali wa klabu za Southampton na Man Utd ambazo tangu mwishoni mwa msimu wa 2015-16 ziliripotiwa kuwa katika hatua za kumgombea mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24.

Msimu uliopita Promes alifanikiwa kuifungia mabao 24 klabu ya Spartak Moscow katika michezo 30 aliyocheza.

Promes, ajiunga na klabu ya Spartak Moscow miaka miwili iliyopita akitokea nchini kwao Uholanzi alipokua akiitumikia klabu ya FC Twente.

Nyongeza ya Mishahara, Ajira Serikalini zapigwa 'Stop'
Walter Zenga Kuziba Nafasi Ya Ronald Koeman