Uongozi wa klabu ya Southampton umeripotiwa kuwa katika harakti za kumuajiri aliyekua mlinda mlango mashuhuri wa timu ya taifa ya Italia Walter Zenga kama mbadala wa Ronald Koeman aliyetimkia Goodson Park juma lililopita.

Kwa mujibu wa gazeti la The The Sun, uongozi wa klabu hiyo umeshaanza kufanya mazungumzo na gwiji huyo wa soka nchini Italia ambaye anaendelea kukumbukwa kutokana na mazuri aliyoyafanya katika michuano mikubwa duniani upande wa klabu pamoja na timu yake ya taifa.

Zenga, mwenye umri wa miaka 58, kwa mara ya mwisho alikua akifundisha soka falme za kiarabu (UAE) katika klabu ya Al-Shaab ambayo aliachana nayo mwezi wa pili mwaka huu.

Mmiliki wa klabu ya Southampton, Katherine Liebherr ameonyesha kuwa tayari kushirikiana na viongozi wengine klabuni hapo, katika harakati za kumpa ajira Zenga ambaye tayari ameshazinoa klabu zaidi ya 10 tangu alipoanza kufanya kazi ya umeneja mwaka 1998.

Klabu zilizowahi kutumikiwa na Zenga ni New England Revolution (1998-1999), Brera (2000–2001), Naţional Bucureşti (2002–2003), Steaua Bucureşti (2004–2005          ), Red Star Belgrade (2005–2006), Gaziantepspor (2006–2007), Al-Ain (2007), Dinamo Bucureşti (2007), Catania (2008–2009), Palermo (2009–2010), Al-Nassr (2010), Al-Nasr (2011–2013), Al Jazira (2013–2014), Sampdoria (2015) pamoja na Al-Shaab (2015–2016).

Quincy Promes Kuwa Mbadala Wa Vardy Emirates Stadium
Mohammed Ibrahim, Muzamir Yasin Watoa Ahadi Kwa Wanamsimbazi