Kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema ametangaza kuwa maandamano yaliyoanza leo marchi 20, 2023 yanayoendelea nchini humo yatakamilika usiku wa manane.

 Huku akiwashukuru Waafrika Kusini kwa kujitokeza kwa wingi kujiunga na maandamano ya ‘National Shutdown’, kiongozi huyo wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) alisema maandamano hayo yamekuwa na mafanikio kinyume na madai kwamba watu hawakujitokeza kama walivyotarajia.

“Asante sana watu wa Afrika Kusini na vikosi vya ardhini vya EFF kwa Ufungaji wa Kitaifa wa EFF kwa amani lakini mahiri ni mwanzo tu sasa, twende nje na tujiunge na mistari ya kashfa, walisema ni siku ya kawaida, lakini unaweza kuona ni akina nani wadanganyifu, ulithibitisha kwa watabiri kwa mara nyingine tena kwamba tunasalia kuwa nguvu pekee ya nidhamu au kushoto ufungaji wa Kitaifa utaisha usiku wa manane, “aliandika kupitia ukurasa wake wa tweet.

Takriban watu 87 walikamatwa Jumatatu asubuhi wakishiriki maandamano hayo. Polisi wa Afrika Kusini walisema kuwa watu hao walikamatwa katika maeneo tofauti ya nchi.

“Kati ya 87 waliokamatwa, 41 walikamatwa Gauteng, 29 Kaskazini Magharibi, 15 katika Jimbo la Free State. Pia kuna watu waliokamatwa katika majimbo mengine kama vile Mpumalanga na Eastern Cape. Taarifa zitatolewa pindi habari zitakapopatikana,” polisi walisema.

Maelfu ya Waafrika Kusini, waliingia mitaani katika maandamano yaliyopewa jina la ‘National Shutdown’ huku nchi hiyo ikikabiliana na masuala, miongoni mwao ukosefu wa ajira, kukatwa kwa umeme na ufisadi wa ovyo. 

Video kadhaa zimesambaa katika mitandao ya kijamii, zikionesha waandamanaji wakimiminika barabarani kwa idadi yao huku kukiwa na madai kwamba wengi walikuwa wameingia mitaani mapema kama 4 asubuhi.

Waandamanaji, wanamtaka Mkuu wa Nchi Cyril Ramaphosa kujiuzulu wakimtuhumu kwa kushindwa kushughulikia masuala hayo.

Waziri Mkuu ataka mikakati kukitangaza Kiswahili Kimataifa
Maandamano ya Odinga yaigia doa mabomu yakirindima