Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya nje wakati wa Serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe.
Kupitia chapisho la ukurasa wake wa twitter na lile lililowekwa katika ukurasa wa Facebook wa Ikulu Mawasiliano, Rais Dkt. Samia amesema kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma.
Amesema, “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi yetu kwa weledi.”
Amesema, Membe pia alikuwa mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi kwa weledi huku akitoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki na kusema Mungu amuweke mahali pema.