Rais wa Rwanda, Paul Kagame amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini na kurejea nchini mwake baada ya kuagwa na wenyeji wake katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax alimsindikiza mgeni wake kama ambavyo alimpokea wakati wa kuwasili kwake akiambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar, Jamal Kassim Ali na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.
Rais Kagame akiagana na Dkt. Tax uwanya wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Viongozi wengine waandamizi wa Serikali
waliomsindikiza ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Charles Karamba na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz.
Rais Kagame na mweyeji wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakiwa katika mazungumzo walikubaliana kuimarisha mambo mbalimbali ya ushirikiano hasa eneo biashara,
miundombinu ya bandari, mradi wa umeme wa Rusumo na suala ya ulinzi na usalama.