Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamesd Shein, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta, ambaye amemaliza muda wake.

Akizungiumza leo leo Novemba 24 Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi John Kijazi, amesema pia Rais Magufuli, amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), akichukua nafasi ya Mariam Joy Mwaffisi.

Mwingine aliyeteuliwa hii leo ni aliyewahi kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akichukua wadhifa huo kwa kipindi cha pili sasa.

Uteuzi wa viongozi wote hao watatu unaanza hii leo

Mzee wa miaka 67 akamatwa kwa kumbaka mjukuu wake
CAF wapeleka fainali Misri

Comments

comments