Rais John Magufuli leo amemteua Hamphrey Polepole kuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Musoma iliyoko mkoani Mara.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu imeeleza kuwa uteuzi huo wa Polepole umeanza rasmi leo, Aprili 18.

“Bw. Hamprey Polepole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,” imeeleza taarifa hiyo.

Mkuu huyo mpya wa Wilaya ya Musoma alianza kufahamika zaidi kwa watanzania kwa mchango wake katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akiwa mmoja kati ya wajumbe wa Tume hiyo iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Mzee Yusuf asema neno kwa Diamond na Ali Kiba, ‘wanaume hawanuniani’
Mtuhumiwa Kesi ya Kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli atoka Rumande