Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt Tulia Ackson na kumteua kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uteuzi huo wa Rais Magufuli umekuja wakati ambapo jina la Dkt. Tulia likiwa miongoni mwa majina matatu yanayopigiwa kura leo na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kumpata mgombea mmoja wa nafasi ya Uspika wa Bunge la 11.

Majina mengine mawili ya waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM jana ni Job Ndugai na Abdallah Ali Mwinyi.

Mugabe: Raila Odinga Akikanyaga Zimbabwe Nitamkamata Na ‘Kumhasi’
Adele aeleza alivyozitosa Ofa Za Makampuni Na Kuimba Kwenye Birthday Za Mabilionea