Mwimbaji wa Uingereza Adele anaendelea kuvunja rekodi na ujio mpya wa wimbo wake ‘Hello’ huku akionekana kuwa lulu ya kuuza bidhaa za makampuni makubwa yanayomfuatilia lakini amekuwa akipiga chini michongo hiyo wanayoiota mastaa wengi.

Msanii huyo ameeleza kwanini amekuwa akiendelea kukwepa paparazzi na kufanya matangazo ya makampuni mbalimbali, katika mahojiano maalum aliyofanya na The Observer.

“Vitu ambavyo nilivyokatalia? Ni kila kitu, unaweza kupata picha. Kwa maelezo tu ni vitu vyote… vitabu, nguo, vyakula, vinywaji, vituo vya mazoezi… hilo linaweza kuwa kituko zaidi. Wanataka niwe kisura wa magari. Midoli, Apps, mishumaa. Ni kama sitaki kuingia kwenye mchongo wa ung’arishaji kucha,” alisema Adele.

Mwimbaji huyo pia aliweka msimamo wake kuwa hawezi kufanya show popote kwa sababu tu analipwa mamilioni ya fedha huku akinyooshea kidole uimbaji kwenye sherehe za kumbukukumbu za siku za kuzaliwa.

“Kunipa Mamilioni ya Pounds kwa ajili ya kuimba kwenye ‘birthday party yako? Ni bora nifanye bure kama nimeamua kufanya,” alisema.

Rais Magufuli Amteua Mgombea Uspika Kuwa Mbunge
Wanafunzi waandamana, wapigwa mabomu ya Machozi