Wanafunzi wa shule ya sekondari Ihungo mjini Bukoba jana walijikuta wakipigwa mabomu ya machozi baada ya kufanya maandamano bila kufuata utaratibu wakipinga ubora wa chakula na mazingira ya shule yao kwa ujumla.

Wanafunzi hao walifanya maandamano kuelekea kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya mji huo kwa lengo la kumueleza matatizo ya shule yao huku wakiwaeleza waandishi wa habari kuwa vyakula wanavyokula havina ubora wa kuliwa na binadamu.

Waliongeza kuwa mbali na vyakula, mazingira ya vyoo inahatarisha maisha yao kwani vyo hivyo haiviko katika hali nzuri na kwamba wanahofia kutokea magonjwa ya mlipuko.

Hata hivyo, wanafunzi hao walionekana kukaidi agizo la Jeshi la Polisi la kuwataka warudi shuleni ili suala lao litafutiwe ufumbuzi hali iliyolilazimu jeshi hilo kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.

Aidha, uongozi wa shule hiyo ulikiri kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa chakula shuleni hapo kwa madai kuwa wazabuni waliokuwa wanaleta chakula wameacha kutokana na kutolipwa madai yao kwa muda mrefu.

“Hadi sasa hivi wazabuni sita wamesitisha kuleta chakula, hawajalipwa muda mrefu kwa hiyo wanasema hawana mitaji ya kuendelea kutoa vyakula,” alisema Mkuu wa Shule hiyo, Philip Boneventula.

Adele aeleza alivyozitosa Ofa Za Makampuni Na Kuimba Kwenye Birthday Za Mabilionea
Diamond Afunika AFRIMMA, Vanessa Naye Ang'ara