Tanzania inaendelea kung’ara kwenye muziki wa Kimataifa ambapo Diamond na Vanessa Mdee jana waling’ara kwenye tuzo za AFRIMMA 2015 zilizotolewa Jana (Novemba 15) jijini Lagos Nigeria.

Diamond alifanikiwa kushinda tuzo tatu ikiwemo tuzo kubwa ya siku ya Msanii Bora wa Mwaka (Best Artist of The Year) akiwashinda Ali Kiba, Wizkid, Yemi Alade, Jose Chameleone, Sarkodie, Flavour na Davido.

Diamond P

Tuzo nyingine mbili alizonyakua ni Wimbo Bora wa Afrika ‘Nasema Nawe’, na Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki.

Kwa upande mwingine, ‘Hawajui’ ya Vanessa Mdee ilimuwezesha kushinda tuzo ya ‘Best African Pop’.

Wanafunzi waandamana, wapigwa mabomu ya Machozi
Polisi watumia mabomu Hospitali ya Bugando Kuwatawanya Chadema