Rais John Magufuli leo amewateua mabalozi wapya watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa watakaoiwakilisha nchi nje ya mipaka.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Ikulu, imeemnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akiwataja mabalozi hao wateule kuwa ni Dkt. Asha Mtengeti Rose Migiro, Mathias Meinrad Chikawe, na Dk. Ramadhani Dau.

Kadhalika, taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Magufuli amempandisha cheo Simon Sirro kutoka cheo cha Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na kisha kumteua kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, akichukua nafasi iliyoachwa na Suleiman Kova aliyestaafu.

Wengine waliopandishwa cheo katika Jeshi la Polisi ni Albert Nyamuhanga, kutoka cheo cha Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi na kuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi kisha kuteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Pia, Robert Boaz Mikomangwa aliyekuwa Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi na sasa ni Kamishna wa Jeshi la Polisi na Rais amemteua kuongoza idara ya Intelijensia.

Mpinzani wa Museveni, Dk. Besigye akamatwa
Wakurugenzi wa MSD watumbuliwa Jibu, wadaiwa kufyeka Bilioni