Rais wa Urusi, Vladmir Putin jana, Machi 14, 2020 alisaini vifungu vya marekebisho ya katiba alivyokuwa amependekeza, ikiwemo kifungu kinachompatia mamlaka ya kuwania mihula mingine miwili.
Mpango huo wa marekebisho ya katiba uliwasilishwa kwenye mahakama ya katiba ya Urusi, ambayo itakuwa na wiki moja ya kupitisha sheria hiyo, itakayoweka upya ukomo wa kikatiba wa Putin kukaa madarakani.
Msemaji katika mahakama ya katiba amesema majaji wameanza kupitia marekebisho hayo, ingawa hakusema lini watatoa maamuzi.
Wamnyonga mtoto wa miezi 9 ili waoane
Putin mwenye umri wa miaka 67, wiki hii aliunga mkono pendekezo la dakika ya mwisho la kuongeza kipengele kitakachomruhusu kurejea mamlakani baada ya muhula wake kikatiba kumalizika mwaka 2024.
Marekebisho hayo pia yanabadilisha usawa wa madaraka, kuongeza jukumu la baraza la ushauri na kuwapa rais na bunge nyenzo zaidi za mamlaka.