Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo  kufuatia kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Hayati William Tate Ole Nasha wakati wa kuaga mwili wa Naibu Waziri huyo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Watanzania  kuaga mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Hayati William Tate Ole Nasha katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Sept 30,2021

Katika hatua nyingine Serikali imesema  kifo cha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Ole Nasha kimetokea baada ya kupata shinikizo la damu.

Katibu mkuu Wizara ya Uwekezaji Profesa Godius Kahyarara amesema ugonjwa huo alikuwa nao tangu mwaka 2014.

Wahamiaji haramu nchini Kenya wasakwa
Kitendawili serikali ya mseto Ujerumani kuteguliwa Oktoba?