Kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Kenya Emilio Mwai Kibaki, Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 2 za maombolezo kuanzia Aprili 29 hadi Aprili 30.

Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari imesema katika maombolezo hayo bendera zote zitapepea nusu mlingoti katika maeneo ya wazi na Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali.

Aidha Rais Samia amewataka watanzani kuungana na Wakenya wote kuomboleza kifo hicho.

Rais Mwai Kibaki Alifariki Aprili 22, 2022 na anatarajia kuzikwa Aprili 30.

90% ya vifo vya Uzazi hutokea katika mazingira ya Hospitali
Magonjwa ya kuambukiza yatapunguzwa na elimu ya afya shuleni