Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku nne Mkoani Kigoma kuanzia tarehe 16-19, 2022 ambapo atakagua na kuweka mawe ya msingi pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa huo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mkuu Mkoa wa Kigoma, Thobias Endengenye amesema ziara hiyo itafanyika katika Wilaya tano za Kakonko, Kibondo, kasulu, Buhigwe na Kigoma na lengo ni kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema, “Rais anategemea kufungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi na atazindua pia miradi ya afya, barabara na maji lakini pia atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani kigoma aidha atapata fursa ya kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali katika wilaya atakazo pitia.”

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Ziara ya Rais Samaia kwa Mkoa kigoma, imeelezewa kuwa na matumaini mapya kwa wakazi wake ambao wanatarajia kupata utatuzi wa changamoto za kibiashara mipakani, ambayo imeendelea kuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.

Katika ziara hiyo, Rais Samia pia atazungumza na wakazi wa Mkoa wa Kigoma kupitia mkutano wa hadhara na hivyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza na kumsikiliza.

Ahmed Ally: Njooni Kwa Mkapa tuweke rekodi mpya
Primero de Agosto yaweka wazi safari ya Dar