Rais wa zamani wa Mali Amadou Toumani Toure, ambaye aliliongoza taifa hilo katika eneo la Sahel kwa miaka 10 kabla ya kuondolewa mamlakani, amefariki leo nchini Uturuki.                                     

Kiongozi huyo wa zamani wa Mali amefariki akiwa na umri wa miaka 72.

Kwa mujibu wa Daktari wake na mwanafamilia ambaye ni mpwa wake, Oumar Toure, Amadou amefariki usiku wa kuamkia leo nchini Uturuki, ambako alikuwa amepelekwa kwa ajili ya matibabu.

Rais huyo wa zamani wa Mali Jenerali AmadouToumani Toure, atakumbukwa kwa jitihada zake za kuleta mageuzi ya kidemokrasia nchini mwake kabla ya kuangushwa kwenye mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 2012.

Serengeti yatunukiwa hifadhi bora Afrika
Rais Ouattara wa Ivory Coast amualika mpinzani wake