Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa mapendekezo kuwa hatua za NATO ndizo za kulaumiwa kwa uvamizi wa Russia dhidi ya jirani yake Ukraine.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema Rais Ramaphosa amepunguza ushawishi wake kama mpatanishi wa mgogoro wa vita nchini Ukraine kwa kawa anaamini silaha na vikwazo vay kiuchumi havitaleta msaada.

Ramaphosa anasema anapendelea mazungumzo badala ya silaha au vikwazo vya kiuchumi akimaanisha vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Russia kutoka Marekani na washirika wa magharibi baada ya uvamizi huo, ambao sasa ni wiki yake ya nne.

Vita hivyo anaamini ghasia nyingi zingeepukika kama NATO ingezingatia maonyo kutoka kwa viongozi na maafisa wake kwa miaka mingi, kwamba upanuzi wake wa mashariki ungesababisha kukosekana kwa utulivu katika eneo hilo.

Ramaphosa anaongeza kuwa Afrika kusini haiwezi kuunga mkono matumizi ya nguvu, na ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Rais wa Afrika kusini alisema nchi yake iliombwa kuwa mpatanishi katika mzozo huo lakini hakumtaja ni nani aliyeiomba Afrika kusini kuingilia kati.

Hersi Said afichua usajili Young Africans 2022/23
Mchengerwa: BASATA wana jukumu la kusimamia Shirikisho la Wasanii