Timu ya Taifa ya Tanzania *Taifa Stars*, itavaana na Tunisia Novemba 13, 2020, kwenye mchezo wa kundi “J” wakuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON 2021), na kisha kurudiana Novemba 17, 2020 jijini Dar es salaam, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka Tanzania *TFF*, mchezo wa kwanza Taifa Stars utakipiga ugenini nchini Tunisia.

Tayari Tanzania imeshacheza michezo miwili ya kundi “J” dhidi ya Equatorial Guinea (ilishinda mabao mawili kwa moja) na ksha ilipambana na Algeria (ilifungwa mabao mawili kwa moja).  

Wakati huo huo kikosi cha Taifa Stars kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya Shiriksho la soka Dunia FIFA.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 11, Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwa leo ni Oktoba 7 zimebaki siku tatu kabla ya mchezo kupigwa.

Kocha wa Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini watapata matokeo mbele ya wapinzani wao.

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa wachezaji waliochaguliwa wapo vizuri na watapambana kupata ushindi.

“Furaha kubwa ya mashabiki ni kupata ushindi hata sisi pia wachezaji tunahitaji ushindi hivyo mashabiki watupe sapoti tutafanya vizuri,” amesema.

Vyama viwili vyajitoa kumuunga mkono JPM
Rais Magufuli ampa pole Zitto Kabwe