Aliyekua nahodha na mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Raúl González Blanco, amethibitisha atastaafu soka mwezi ujao, baada ya kuutumikia mchezo huo tangu mwaka 1987.

Raul, ametangaza dhamira hiyo akiwa nchini Marekani, ambapo shughuli zake za kucheza soka zipo nchini humo katika klabu ya New York Cosmos, ambayo ilimsajili Oktoba 30 mwaka 2014.

Raul mwenye umri wa miaka 38, amesema amefanya maamuzi ya kujitayarisha kukaa pembeni, baada ya kujifikiria kwa muda mrefu na kuona muda wake wa kucheza soka umefikia ukingoni.

Amesema mwaka jana wakati akijiunga na klabu ya New York Cosmos, akitokea nchini Qatar kwenye klabu ya Al Asaad, aliweka dhamira ya kujipima kwa kuona kama angeweza kucheza kwa mwaka mmoja zaidi.

Amesema pamoja na kuafanya maamuzi hayo kwa lengo la kujiweka pembeni, pia anaamini wakati wa kukaa karibu na familia yake watoto watano umewadia, baada ya kuishi nao kwa muda mchache kutokana na purukushani za maisha ya soka.

Raul, ana watoto wanne wakiume ambao ni Jorge, Hugo, Héctor na Mateo (Mapacha) pamoja na María ambaye ni wa kike.

Raul ataendelea kukumbukwa na mashabiki wa soka nchini Hispania hususan wale wa klabu ya Real Madrid ambao walishuhudia gwiji huyo akiitumikia klabu yao katika michezo ya 550, na kufunga mabao zaidi ya 450.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Hispania, Raul, pia ameweka historia itakayokumbukwa kwa kucheza michezo 102 na kufunga mabao 44.

Platini Atengenezewa Mazingira Ya Kueleweka
Ujenzi Wa Barabara Za Juu ‘Flyover’ Kuanza Mwezi Ujao, Magufuli Anena