Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya kimichezo (CAS) imeipunguzia adhabu klabu ya Real Madrid, kwa kuwaamuru kufanya usajili itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Real Madrid walikata rufaa katika mahakama hiyo, siku chache baada ya kuadhibiwa na shirikisho la soka duniani FIFA kwa kutofanya usajili hadi Januar1 2018.

Hukumu hiyo kwa Real Madrid inaendelea kuwanyima nafasi ya kufanya usajili wakati wa majira ya kiangazi (Januari 2017).

“Mahakama ya usuluhisi (CAS) inaifahamisha klabu ya Real Madrid C. F. kuwa huru kufanya usajili itakapofika mwishoni mwa msimu huu, baada ya kupitiwa kwa rufaa yao na kubaini adhabu waliokua wamepewa na FIFA ilikua kubwa kuliko makosa waliyoyafanya,

“Tumebaini usajili ambao ulikwenda kinyume na taratibu za FIFA uliingiza klabu hii katika hatia kubwa, lakini sio kwa kiwango cha adhabu iliyowaangukia, wataendelea kutumia adhabu ya kutofanya usajili kwa mwezi Januari 2017, lakini watakua huru kuanzia mwishoni mwa msimu huu.” Ilieleza taarifa ya CAS.

Mahakama yawafutia kesi viongozi wa Chadema
Karamoko Dembele Avaa Jezi Ya England