Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imesema raia zaidi ya laki tatu na elfu sitini waliuawa kati ya tarehe 1 mpaka 31 ya mwezi Machi mwaka 2022 nchini Syria, kutokana na vita inayoendelea nchini humo ikiwa ni idadi kubwa ya vifo tangu kuanza kurekodiwa taarifa za mauaji nchini Syria.
Ripoti hiyo ya Baraza la Haki za Binadamu iliyotolewa hii leo Juni 29, 2022 jijini Geneva nchini Uswisi, imeeleza kurekodi taarifa za vifo vya raia 143,350 kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo majina yao kamili na eneo la kifo.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Michelle Bachelet amesema idadi ya vifo nchini Syria katika kipindi cha miaka 10 ni takriban asilimia 1.5 ya idadi ya watu wa taifa hilo.
“Takwimu hizi za waathirka katika ripoti hii sio tu nambari bali zinawakilisha binadamu mmoja mmoja. Madhara ya mauaji ya kila mmoja wa raia hawa 306,887 yamekuwa na athari kubwa na yamerudisha nyuma familia na jamii walizokuwa nayo,” amesema Bachelet.
Ameongeza kuwa, uchunguzi unaofanyika na taarifa zinazorekodiwa na Umoja wa Mataifa na wadau wengine zinasaidia kwa familia hizo na kusema uchambuzi huo pia utatoa hisia za wazi zaidi ya ukali na ukubwa wa mzozo nchini humo.
“Kazi ya mashirika ya kiraia na Umoja wa Mataifa katika kufuatilia na kuweka kumbukumbu za vifo vinavyotokana na migogoro ni muhimu katika kuzisaidia familia na jumuiya hizi kubaini ukweli, kutafuta uwajibikaji na kutafuta masuluhisho madhubuti,” ameongeza Bachelet.
Kamishna huyo wa haki za binadamu, katika kuonesha ukubwa wa mzozo nchini Syria ameeleza kuwa takwimu zilizotolewa leo ni watu waliouawa katika matukio ya moja kwa moja ya opesheni za vita na kwamba idadi hiyo haijumuishi raia waliokufa kutokana na kukosa huduma za afya, chakula, maji safi na haki nyingine muhimu za binadamu, ambazo hazijatathminiwa.