Aliyekua beki wa klabu za Liverpool na West Ham Utd, Rigobert Song amekimbizwa hospitalini akiwa katika hali mahututi baada ya kuugua kiharusi.

Song, mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni mjomba wa aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, West Ham na Charlton Athletic Alex Song, alichezea timu ya taifa ya Cameroon katika michezo 137.

Taarifa zinasema alikuwa nyumbani kwake Odza, Yaounde alipopatwa na kiharusi na akakimbizwa hospitalini siku ya Jumapili.

Song, ambaye alikuwa nahodha wa Indomitable Lions, ndiye kocha mkuu wa timu ya taifa ya Chad, kazi aliyokabidhiwa mwishoni mwa mwaka jana.

Ndiye mchezaji aliyechezea timu ya taifa ya Cameroon michezo mingi zaidi.

Wachezaji wengine nyota wa Cameroon, akiwemo Samuel Eto’oo, wamemtakia afueni ya haraka.

“Namtakia ndugu yangu mkubwa ujasiri na uponaji wa haraka,” Eto’o ameandika kwenye Twitter na Instagram.

Song

Song alicheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa dhidi ya Mexico mwaka 1993 na alikuwa nahodha wa Cameroon kwa miaka 10, na baadae alimuachia Samuel Eto’o mwaka 2009.

Alistaafu soka ya kimataifa 2010 baada ya kucheza Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

Video: Tamko la Waziri Mkuu kuhusu wadaiwa sugu taasisi za Serikali
Samuel Eto'o Atoka Kifungoni