Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kumshikilia Issack Habakuki Emily kwa kosa la kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kupitia mtandao wa Facebook, walio-like comment yake wanadaiwa kusakwa na Jeshi la Polisi.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutoa lugha chafu dhidi ya Rais kupitia comment yake kwenye mada iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook ikiwataka watu kutoa maoni yao kwa namna wanavyoweza kuufananisha uongozi wa Rais Magufuli na ule wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika serikali ya awamu ya Kwanza.

Taarifa kutoka  Arusha zilizoandikwa pia na aliyewahi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostino (SAUT), Malisa Godlisten akitumia vyanzo vya jijini humo, zimeeleza kuwa watu hao walio-like wanatafutwa kwa ajili ya kutoa ushahidi kuhusu ‘comment’ hiyo ya mtuhumiwa ambayo wao walii-like.

Mtuhumiwa anashtakiwa kwa kuvunja sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Jumla ya watu 13 wali-like comment hiyo. Kuwa makini unapotumia mitandao ya kijamii. Bado Jeshi la Polisi mkoani humo hazijatoa taarifa rasmi kuhusu taarifa za kuwatafuta watu hao.

 

Symbion, Tanesco waburuzwa mahakamani wakidaiwa mabilioni
Fahamu sakata la Helikopita ya Polisi kutumwa Pochi ya Gavana Nyumbani kwake