Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya Kufua Umeme ya Kimarekani ya Symbion Ltd zimeburuzwa mahakamani zikidaiwa $28 (zaidi ya shilingi bilioni 60) kwa kukodi mitambo.

Kampuni ya Rental Solutions and Services LLC imefungua kesi dhidi ya taasisi hizo katika Mahakama Kuu ikiiomba mahakama hiyo kuamuru Symbion kulipia gharama za matumizi ya mitambo iliyoikodisha kwa kampuni hiyo.

Tanesco imetajwa kama mshitakiwa wa pili huku mlalamikaji akiitaka Mahakama kuamua kuwa maamuzi itakayoyatoa yatakuwa na madhara kwa shirika hilo pia moja kwa moja.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba aliwaambia waandishi wa habari kuwa hana taarifa juu ya mashtaka hayo lakini pia shirika hilo halihusiki na biashara ya kukodishiana mitambo kati ya Symbion na mlalamikaji.

“Huo mkataba ulisainiwa na hao wawili [Symbion na Rental Solutions and Services LLC], sisi sio sehemu ya mkataba wao,” alieleza Mramba.

DART YAHIMIZWA KUELIMISHA WAKAZI WA DAR
Ripoti: Walio-‘like’ coment ya aliyetoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli wasakwa na Polisi