Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu imebaini kuongezeka kwa vitendo vya ukatili na ubakaji Jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na mtafiti wa kituo hicho, Paul Mikongoti alipokuwa akisoma ripoti hiyo mbele ya wadau mbalimbali wa haki za binadamu.

Amesema kuwa matukio hayo yamefanyika katika kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu, ambapo watoto 2,571 walibakwa katika mkoa wa Dar es salaam.

“Wazazi wengi wameelekeza nguvu zao kwenye utafutaji mali kuliko kujali hali za familia inaendaje, kitu ambacho kimekuwa kikiwaathiri watoto kwa kukosa uangalizi mzuri, hata kama mtoto atakuwa amefanyiwa kitendo cha kikatili mzazi hawezi kuelewa,”amesema Mikongoti.

Hata hivyo, ameongeza kuwa matukio ya unyanyasaji wa wanawake unaonyesha kuwa ni tatizo kubwa hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa hivyo inahitajika nguvu ya ziada ya utoaji elimu.

?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 4, 2017
Video: Seif asema heri CCM, Wanaokata rufaa vyeti feki waonywa