Nyota wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney amekutwa na hatia ya kuendesha gari akiwa ametumia kilevi katika kesi iliyosomwa hii leo kwenye mahakama ya Stockport Magistrates Kusini mwa jiji la Manchester.

Rooney alikuwepo mahakamani hapo ambapo amekutana na hukumu inayomtaka kufanya kazi za jamii kwa muda wa saa 100 pamoja na kuripoti mahakamani kwa miezi 12 huku adhabu kubwa ikiwa ni kutoendesha gari kwa miaka miwili

Aidha, nyota huyo alikamatwa asubuhi ya Septemba 1 akiwa anaendesha gari mitaa ya nyumbani kwake Prestbury, Cheshire ambapo vipimo vya wana usalama wa barabarani vilionyesha ametumia kilevi kiasi cha 104mg

Hata hivyo, Rooney mwenye umri wa miaka 31 ameomba msamaha kwa uongozi wa klabu yake ya Everton pamoja na mashabiki wa klabu hiy, huku Eveton itamkata Rooney mshahara wa wiki mbili. Pia adhabu yake ya kutoendesha gari inaweza kupunguzwa hadi wiki 24 endapo atapata mafunzo maalum ya usalama barabarani kufikia Februari 2, 2019.

Polisi yakamata waandamanaji nchini Uganda
Aliyekuwa Waziri wa Awamu ya Nne apoteza ndugu 13 katika ajali ya gari