Jeshi la Polisi nchini Uganda limewakamata vijana 14 wa kundi la ‘Jobless Brotherhood’ kwa tuhuma za kufanya maandamano kupinga marekebisho ya katiba kuhusu ukomo wa urais.

Tukio hilo limetokea hii leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala, ambapo vijana waliokamatwa wamepelekwa katika kituo kikuu cha polisi, ili kuweza kuhojiwa sababu za kufanya maandamano.

Aidha, kwa mujibu wa kikundi hicho wamefanya maandamano hayo huku wakisambaza vipeperushi vyenye ujumbe wa kupinga kitendo hicho cha kufanya mchakato wa kubadili katiba ya nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mbunge, Muhhamad Nsereko ambaye ni miongoni mwa watu wanaopinga suala hilo, amesema kuwa vijana hao wamechukuliwa kwa ajili ya mahojiano hapo kesho na wataendelea kufanya hivyo kwa manufaa ya taifa lao.

“Katiba haitabadilishwa, haturudi nyuma kwa hili licha ya kukamatwa, wanatutaka tuwe wazalendo na kuitetea nchi yetu, tusiogopeshwe , tuendelee na safari kuijenga nchi yetu”, amesema Nsereko.

Hata hivyo, Wabunge nchini Uganda wameanza kujadili mchakato wa kubadilisha katiba itakayomruhusu Rais Yoweri Museveni kubakia madarakani kwa muda mrefu zaidi, kitendo ambacho kimeonekana kupingwa vikali na baadhi ya wananchi.

Askari anayejiita Faru John ahojiwa
Rooney akumbana na hukumu baada ya kukiri kosa