Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa ametamba kuvunja Rekodi ya Young Africans kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguuko wa Sita.

Miamba hiyo itapapatuana Oktoba 03, Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku Young Africans ikiendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu tangu msimu uliopita.

Kocha Mkwasa ambaye aliwahi kuitumia Young Africans kama Mchezaji, Kocha Mkuu na kisha Katibu Mkuu amesema anaendelea kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo huo, huku akimini wachezaji wake wataweza kuvunja rekodi ya wapinzani wao.

Amesema anatambua Young Africans imebadilika na ina kikosi imara tofauti na ilivyokua misimu mitatu iliyopita, lakini hilo halimpi shida, zaidi ya kuamini maandalizi anayoyafanya yatakua mkombozi wa kuvunja Rekodi ya wapinzani.

“Sikatai Young Africans kwa sasa imebadilika sana tofauti na ile ya misimu mitatu iliyopita, lakini hili ni soka, naamini wao wanajipanga na sisi tunajipanga na tupo tayari kuvuruga rekodi yao,” amesema Mkwasa

Hadi sasa Young Africans imeshacheza michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikishinda mitatu na kutoka sare mchezo mmoja, huku Ruvu Shooting ikishuka dimbani mara nne, imeshinda michezo miwili na kupoteza miwili.

Juma Mgunda aitanguliza Dodoma Jiji FC
Al Hilal yamnyima usingizi Fiston Mayele